Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel awasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza stoo Ngara

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Godwin Mollel, amewasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza Stoo wa Hospitali ya Wilaya ya Ngara ya Nyamiaga mkoani Kagera ili kupisha uchuguzi. Watumishi hao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na upotevu wa dawa za mamilioni ya fedha zilizoletwa na Serikali kwa ajili ya wananchi.